Wakiongea kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wapatao 71 wamesema, Tanzania imepiga hatua kubwa katika utunzaji wa kumbukumbu za historia ya ukombozi wa mataifa ya Afrika na kuzitaka nchi jirani hasa za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuja kujifunza na kuona historia hiyo ilivyohifadhiwa na namna inavyorithishwa katika jamii.