Majukumu Ya Kituo

Majukumu Ya Kituo

Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kitakuwa na majukumu yafuatayo:

i.    Kuratibu ushirikiano baina ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, taasisi za kikanda na kimataifa pamoja na wadau mbalimbali wa urithi;
ii.    Kuratibu uanzishwaji wa Makao Makuu ya Kituo Kikuu cha Uhifadhi wa Urithi wa Ukombozi wa Afrika nchini Tanzania;
iii.    Kuanzisha na kusimamia mifumo ya kitaalamu ya ukusanyaji, uwekaji kumbukumbu, uhifadhi wa kidijitali na usimamizi wa taarifa za Urithi wa Ukombozi wa Afrika;
iv.    Kuratibu uandaaji na uchapishaji wa vitabu vya historia ya ukombozi wa Afrika; 
v.    Kuandaa na kusimamia uandaaji wa miongozo na taratibu za utambuzi na usimamizi wa maeneo, vitu, vielelezo na nyaraka za Urithi wa Ukombozi wa Afrika;
vi.    Kuratibu utambuzi, uwekaji wa kumbukumbu na utafiti wa maeneo muhimu ya kihistoria ya ukombozi wa Afrika pamoja na kuyahifadhi na kuyaendeleza;
vii.    Kuanzisha na kuendesha mifumo ya programu za elimu, maonesho, maktaba, nyaraka na majukwaa ya kidijitali kwa ajili ya kuelimisha umma kuhusu historia ya ukombozi wa Afrika;
viii.    Kuratibu na kuendesha makongamano, warsha, semina, maonesho, mijadala na shughuli nyingine za kitaaluma kuhusu Urithi wa Ukombozi wa Afrika;
ix.    Kukuza ushirikiano na kujenga mitandao ya kitaifa, kikanda na kimataifa kati ya taasisi za urithi, vyuo vikuu, vituo vya utafiti na mashirika mengine yanayohusika na historia ya ukombozi wa Afrika;
x.    Kuratibu programu za kuenzi mashujaa na mashujaa wanawake wa harakati za ukombozi wa Afrika pamoja na kuhifadhi simulizi, kumbukumbu na ushuhuda wao kwa ajili ya vizazi vijavyo;
xi.    Kuhamasisha matumizi ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika katika elimu, utafiti, utalii wa urithi, ubunifu na maendeleo ya kiuchumi na kijamii;
xii.    Kuhamasisha na kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi, taasisi za umma, washirika wa maendeleo, asasi za kiraia na wadau wengine katika uwekezaji, uhifadhi na uendelezaji wa Urithi wa Ukombozi wa Afrika;
xiii.    Kuwezesha uanzishwaji na uimarishaji wa Matawi ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika katika Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika pamoja na kuratibu ushirikiano baina ya matawi hayo;
xiv.    Kujenga na kuendeleza uwezo wa kitaalamu wa watumishi wa Kituo, wataalamu wa urithi na wadau wengine kupitia mafunzo, kubadilishana uzoefu, utafiti shirikishi na programu za maendeleo ya kitaaluma.

lbl_need_any_help