Nyumba ya Hayati Eduardo Mondlane

Nyumba ya Hayati Eduardo Mondlane

Tanzania
Nyumba ya Hayati Eduardo Mondlane
Nyumba ya Eduardo Mondlane – Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Nyumba ya Eduardo Mondlane ni moja ya majengo muhimu ya kihistoria yaliyopo ndani ya Kambi ya Ukombozi ya Farm 17 iliyopo Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Tanzania. Eneo hili ni sehemu ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika (ALHC), kinachohifadhi maeneo yenye uhusiano na mapambano ya ukombozi wa Afrika.

Nyumba hii imepewa jina la Eduardo Mondlane, aliyekuwa rais wa kwanza na mwanzilishi wa chama cha FRELIMO (Frente de Libertação de Moçambique) na mmoja wa viongozi muhimu wa harakati za ukombozi wa Msumbiji.

Katika kipindi cha vita vya ukombozi vya miaka ya 1960 na 1970, Farm 17 ilitumika kama kituo cha kimkakati ambapo Mondlane pamoja na viongozi wengine wa FRELIMO waliratibu shughuli za kijeshi na kisiasa dhidi ya ukoloni wa Ureno. Baada ya kuuawa kwake mwaka 1969, urithi wake uliendelea kuwa na uhusiano mkubwa na Nachingwea, ambapo wafuasi wake waliendelea kupata mafunzo na kuendesha mipango ya harakati za ukombozi.

Nyumba Na. 84B, iliyopo Mlalakuwa, mkabala na Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ndipo mahali yalipomsibu mauti kiongozi wa kwanza wa FRELIMO hayati Eduardo Mondlane mwaka 1969. Nyumba ipo:

Barabara ya “Old Bagamoyo”

Serikali ya Mtaa Mlalakuwa

Kata ya Kawe

Tarafa ya Kawe

Manispaa ya Kinondoni

lbl_need_any_help